KILIMO BORA CHA MBAAZI MUDA MFUPI
  • By NICHOLAUS.SHOKELA
  • Leaflets
Publication Year : 2022

Author(s) : Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)-Kituo cha Ilonga

Mbaazi ya muda mfupi hukomaa kati ya siku 120 hadi 125 maeneo ya Morogoro, Tanga, Pwani, Mtwara na Dar es Salaam. Katika ukanda wa juu kwenye baridi, mbaazi za muda mfupi hukomaaa kwa muda mrefu zaidi ya siki 120. Mbaazi za asili hukomaa kati ya siku 210 hadi 270. Mbaazi za muda mfupi hutoa mavuno mengi zaidi ya zile za asili iwapo zitalimwa kwa kuzingatia maelezo ya kitaalamu.