KILIMO BORA CHA MAHARAGWE KAWAIDA BUSH.
  • By MOSSES.BAYINGA
  • Leaflets
Publication Year : 2015

Author(s) : Idara ya Utafiti wa Maharagwe Kitaifa: Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Chakula Selian.

Maharagwe ni zao muhimu katika kanda ya kaskazini na nchi nzima kwa ujumla. Hutumika kama chakula kwa kutowelea vyakula mbalimbali kama ugali, wali, makande na kadhalika pia majani yake hutumika kama mboga za majani. Hivi sasa maharagwe yameanza kuwa zao la biashara hasa katika maeneo yale ambayo hayana zao la kudumu la biashara, na majani yake yakishakauka yamekuwa chanzo muhimu cha kumuongezea mkulima kipato ambapo hufungwa na kuuzwa kwa bei ya juu kama chakula cha mifugo. Wakulima wengi wamekuwa wanapata mavuno haba kutokana na sababu mbalimbali mojawapo zikiwa ni kutokutumia mbegu Bora za maharagwe , kutokuzingatia njia mbalimbali za matunzo zinazopendekezwa, kutokufahamu namna ya kuwadhibiti wadudu na magonjwa ya maharagwe na hifadhi. Kijarida hiki kidogo kina nia ya kutoa ushauri kwa ujumla kwa wakulima wa maharagwe ili kuongeza chakula bora cha mifugo na ziada kwa kuuza ili kuinua kipato cha mkulima.