Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

TARI, Chuo Kikuu cha Kilimo Shandong kushirikiana katika tafiti, ubunifu wa teknolojia na kubadilishana wataalamu.
15 Apr, 2026
TARI, Chuo Kikuu cha Kilimo Shandong kushirikiana katika tafiti, ubunifu wa teknolojia na kubadilishana wataalamu.

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imepokea ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Shandong cha nchini china katika ziara maalum iliyofanyika tarehe 14 Aprili 2026, jijini Dodoma, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika sekta ya kilimo.

Katika ziara hiyo, ujumbe ulitembelea vituo vya utafiti vya Makutupora na Hombolo ili kujionea shughuli za utafiti na teknolojia zinazotekelezwa na TARI.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Thomas Bwana, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukuza ubunifu na kuongeza tija katika kilimo. Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu, Dkt. Deusdedith Mbanzibwa, alieleza maeneo ya kipaumbele ya ushirikiano ikiwemo bioinformatics, kubadilishana wataalamu, tafiti za pamoja na uhaulishaji wa teknolojia kwa wakulima.

Kwa upande wake, Rais wa Chuo Kikuu cha Shandong Prof. Leng Changjian, alieleza dhamira ya kuimarisha ushirikiano huo, akibainisha mafanikio ya China katika matumizi ya teknolojia za kisasa za kilimo.

Pande zote zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika tafiti, ubunifu wa teknolojia, kubadilishana wataalamu, pamoja na kuanzisha majukwaa ya pamoja ya utafiti hususan katika bayoteknolojia na molecular science.