Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

Tehama

Kitengo cha TEHAMA na Takwimu kinatoa mwongozo na utaalamu wa kiufundi kuhusu matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuboresha utoaji wa huduma na uchambuzi wa takwimu. Kinatekeleza sera za TEHAMA na e-Serikali, kinaunga mkono ukuzaji na matengenezo ya mifumo ya programu, kinashughulikia ununuzi wa vifaa na programu za TEHAMA, kinasimamia mawasiliano ya barua pepe kupitia mtandao wa LAN na WAN, na hufanya tafiti kutambua maeneo ambapo TEHAMA inaweza kuboresha ufanisi wa taasisi.