WAKULIMA WAENDELEA KUCHANGAMKIA KILIMO SHADIDI CHA MPUNGA.
Wakulima wa zao la mpunga nchini wameendelea kujifunza na kulima kwa kufuata kanuni za kilimo shadidi cha mpunga kilichoboreshwa ambacho pamoja na mambo mengine kinahimiza matumizi ya mbegu kidogo, maji kidogo lakini mavuno yanakuwa mengi.
Kauli hiyo imetolewa na Mtafiti wa zao la Mpunga kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Atugonza Bilaro katika siku ya Mkulima wa zao la Mpunga iliyofanyika mapema wiki hii katika skimu za Ilonga Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro na Skimu ya Mariwanda Wilaya ya Bunda Mkoani Mara.
Dkt. Bilaro ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Kilimo shadidi cha Mpunga alisema kipindi mradi unaanza mwaka 2022 ulilenga kuwafikia wakulima elfu mbili katika Halmashauri tano za Bunda, Chalinze, Iringa Vijijini, Kilombero na Mbarali lakini hadi sasa wamefikia zaidi ya wakulima elfu sita wa mpunga katika maeneo mbalimbali yanayolima zao hilo nchini.
Akieleza kuhusu kilimo shadidi cha Mpunga Dkt. Bilaro alisema ni teknolojia inayofuata kanuni kuu sita ambazo zinalenga kumuongezea mkulima tija huku gharama za uzalishaji zikipungua.
Dkt. Bilaro alitaja kanuni za kilimo shadidi cha mpunga kuwa ni kupanda miche michanga ya siku 8-14 kutoka kwenye kitalu Mkeka, kupanda mche mmoja moja, kuingiza maji shambani pale yanapohitajika kwa kutumia kifaa cha (AWD).
Kanuni zingine ni kutumia kifaa cha (LCC) kupima mmea kama unahitaji kuweka mbolea badala ya kuweka kwa kubahatisha, kupanda kwa mraba wa sentimita ishirini na tano shina hadi shina na mstari hadi mstari pamoja na kupalilia kwa kutumia vipalizi.
“Kilimo shadidi tunalenga kusaidia mkulima kuongeza tija ukizingatia uwepo wa athari za mabadiliko ya tabia nchi na matokeo mengine ikiwemo ongezeka la watu lakini maeneo ya uzalishaji hayaongezeki hivyo kilimo hiki kinahimiza uzalishaji mkubwa katika eneo dogo huku gharama za uzalishaji huo mkubwa zikipungua mara dufu kulinganisha na kilimo cha kawaida” alisema Dkt. Bilaro.
Akieleza manufaa aliyopata mkulima wa mpunga skimu ya Mariwanda Bi. Dorica Biseko alisema tangu aanze kulima kilimo shadidi mavuno yameongezeka kutoka wastani wa gunia kumi na tano kwa ekari alizokuwa akipata pindi analima kilimo cha mazoea hadi kufikia wastani wa gunia thelathini na tano kwa ekari katika kilimo shadidi.
Pia manufaa kama hayo anayataja Mkulima skimu ya Ilonga Bwana, Godfrey Paschal aliyesema katika kilimo cha mazoea alikuwa akivuna wastani wa gunia nane hadi kumi kwa ekari lakini tangu apate mafunzo kutoka TARI katika kilimo shadidi anavuna wastani wa gunia thelathini na tano kwa ekari.
Naye mkulima wa mpunga skimu ya Ilonga Bwana Alex Mwinuka alitaja faida nyingine kuwa ni pamoja na matumizi ya mbegu kidogo ambapo zamani anasema alikuwa akitumia zaidi ya kilogramu kumi kupanda ekari moja lakini baada ya kupata mafunzo kutoka TARI kupitia kitalu mkeka anapanda ekari moja kwa kilogramu mbili.
Akizungumza katika skimu ya Mariwanda Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mheshimiwa Aswege Kaminyoge ameipongeza TARI kwa kupeleka teknolojia hiyo na kuagiza maafisa ugani wa Wilaya kuhakikisha teknolojia hiyo inawafikia wakulima wengi zaidi ili kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, Halmashauri na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Afisa tarafa ya Kimamba, Bi. Sabina Lucas akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, pia alipongeza TARI kwa kufikisha elimu ya kilimo shadidi cha Mpunga kwa wakulima na kusema hatua hiyo inachangia sula la usalama wa chakula nchini.