Uhaulishaji wa Teknolojia na Mahusiano
Idara hii inaweka mkazo mkubwa katika kuendeleza, kupanua, na kusambaza teknolojia za kilimo, ubunifu, na mbinu bora za kilimo. Juhudi hizi zinalenga kuhakikisha matumizi mapana ya teknolojia za kilimo na matumizi bora ya matokeo ya utafiti ili kuongeza uzalishaji wa kilimo, tija, na kipato cha wakulima. Idara ya Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushirikiano imegawanyika katika sehemu kuu mbili:
1. Uhaulishaji wa Teknolojia, Mahusiano na Biashara.
Sehemu hii inawajibika kwa:
-
Kuwezesha uhaulishaji wa teknolojia za kilimo zinazofaa, ubunifu na mbinu bora za usimamizi kwa wakulima na wadau wengine.
-
Kuratibu ukusanyaji, uhifadhi na usambazaji wa taarifa juu ya teknolojia za utafiti wa kilimo miongoni mwa watafiti na wadau wengine.
-
Kusaidia na kusimamia utekelezaji wa maonesho ya kilimo, maonesho ya kibiashara, makongamano, warsha, mikutano ya kitaaluma, na ziara za mafunzo.
-
Kusaidia vituo vya utafiti katika kukuza na kuendeleza biashara za teknolojia na ubunifu wao.
-
Kuandaa Hati za Makubaliano (MoUs) kwa ajili ya kuanzisha na kuimarisha ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kikanda, na kimataifa.
2. Usimamizi wa Maarifa na Mawasiliano
Sehemu hii inawajibika kwa:
-
Kuhifadhi na kusambaza teknolojia na ubunifu wa kilimo.
-
Kubadilisha na kupanua matumizi ya teknolojia ili kufikia watumiaji wengi zaidi.
-
Kubaini mbinu, mikakati, na njia za kuboresha mawasiliano.
-
Kuanzisha na kudumisha hifadhidata za maarifa ya kisayansi na teknolojia zilizoasiliwa.
-
Kuandaa zana na mbinu za utafiti kwa ajili ya kubaini fursa za utafiti na kufuatilia utekelezaji wake.
-
Kubuni na kutekeleza mikakati ya mawasiliano inayolenga umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari, vikiwemo vya kuchapisha, sauti, picha, mikutano ya waandishi wa habari, na majukwaa mengine ya kielektroniki.