Adoption and Impact studies
Adoption and Impact studies
Ufuatiliaji wa Upitishaji na Athari za Teknolojia
Kitengo cha Uchumi wa Jamii hushughulikia tafiti za upokelewaji wa teknolojia (adoption) na athari (impact) za aina mbalimbali za mazao na teknolojia za kilimo. Tafiti hizi huchambua jinsi wakulima na wadau wengine wanavyotumia teknolojia mpya za kilimo na sababu zinazochangia au kuzuia matumizi yake.
Pia, tafiti hizi hupima athari za kiuchumi, kijamii, na kimazingira za teknolojia hizo, na kutoa mrejesho (feedback) wa kuboresha utafiti, kusaidia katika utungaji wa sera, na kuwezesha maamuzi sahihi ya uwekezaji katika sekta ya kilimo.