TARI MIKOCHENI
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania – Mikocheni (TARI-Mikocheni) ni mojawapo ya vituo 20 vya utafiti chini ya TARI. Iliundwa mwezi Machi 1996 kama hatua ya kudumisha na kuanzisha rasmi shughuli za utafiti na maendeleo ya nazi zilizoendeshwa na Mpango wa Taifa wa Maendeleo ya Nazi (NCDP) wa wakati huo. NCDP ilianzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwaka wa fedha 1979/80 kwa lengo la kukuza uzalishaji na matumizi ya nazi nchini. Mpango huo ulifunika pwani nzima ya Tanzania pamoja na Kisiwa cha Zanzibar.
TARI-Mikocheni ina majukumu mawili, yaani kufanya na kukuza utafiti kwa ajili ya maendeleo ya sekta ndogo ya nazi, pamoja na kukuza utafiti na matumizi ya bioteknolojia ya kilimo kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Taasisi hii ni mojawapo ya sub-centres pamoja na TARI Kibaha, zote zikipo chini ya Kituo cha TARI Mlingano Kanda ya Mashariki. Ofisi kuu ya kituo iko Dar es Salaam, Mikocheni B, Ploti 22 kando ya Barabara ya Coca Cola.
Kituo kina vituo vidogo viwili, Chambezi na Mkuranga, ambapo shughuli nyingi za utafiti zinafanyika. Kituo cha kwanza kiko karibu kilomita 55 kaskazini mwa Dar es Salaam karibu na Mji wa Bagamoyo kwenye latitude S 6.520 na longitude E 38.910, wakati kituo kidogo cha pili kiko kwenye latitude S 7.120 na longitude E 39.200, karibu kilomita 50 kusini mwa Dar es Salaam.