NJIA ZA UHAULISHAJI
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania hutumia njia mbalimbali za kufikisha matokeo ya utafiti na teknolojia za kilimo kwa wakulima, wafanyakazi wa ugani, watunga sera, na wadau wengine. Njia hizi hujumuisha mbinu mbalimbali za jadi na za kisasa ili kuwafikia watu wengi zaidi na kuleta matokeo yenye nufanisi.
Njia hizo ni pamoja na:
-
Mashamba darasa na Siku za Wakulima
-
TARI huanzisha mashamba darasa pamoja na mashambani ya mfano na kuwezesha wakulima na wadau kujifunza kwa kuona mbinu za kilimo bora kwa vitendo.
-
Siku ya Mkulima huandaliwa kwa lengo la kuonyesha matokeo ya utafiti pamoja na ufanisi wa mbinu za kilimo bora shambani. Pia, huimarisha ushirikiano kati ya wakulima na watafiti.
-
-
Mafunzo na kujengea uwezo
-
TARI hutoa mafunzo kwa wakulima na wadau kuhusu teknolojia mpya na kanuni za kilimo bora. wadau hao ni pamoja na wafanyakazi wa ugani, vijana, na vikundi vya wanawake. pia huwajengea uwezo kupitia warsa, makongamano, mikutano
-
huandaa miongozo mbalimbali inayosimamia na kuratibu utekelezaji wa shuguli za utafiti na uhaulishaji teknolojia.
-
-
Vyombo vya Habari
-
TARI hushirikiana na vyombo vya habari kamavile luninga, redio, magazeti, majarida kutoa elimu kuhusu kilimo bora na kuhamasisha matumizi ya teknolojia bora za kilimo.
-
Kwa kupitia vipindi vya redio na luninga, makala, habari, video, picha, hadithi za mafanikio hujenga uelewa miongoni mwa wadau hususani wakulima ili kuchochea matumizi ya teknolojia hizo.
-
-
Mitandao ya Kijamii na Mijadala ya Kidigitali
-
TARI hutumia mitandao kama Facebook, X (Twitter), YouTube, na Instagram kusambaza taarifa za utafiti kwa wadau
-
Tovuti ya TARI ni kituo kikuu cha kuchapisha machapisho, matokeo ya utafiti, na nyaraka za kupakua.
-
-
Machapisho ya kuelimisha na kuhamasisha wakulima na wadau
-
Elimu kuhusu kilimo bora husambazwa kupitia vipeperushi, mabango, vijitabu, ambavyo huandikwa kwa lugha rahisi na rafiki kwa wakulima na wadau kuelewa.
-
-
Maonyesho ya Kilimo na Maonesho ya Biashara
-
TARI inatumia fursa ya maonesho mbalimbali ya kitaifa na kikanda kama Sabasaba, Nanenane, Maonesho ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), Siku ya Cahakula Duniani, Wiki ya Mazingira na mengineyo kuonesha teknolojia mpya ikiwemo mbegu bora, bidhaa za mazao zilizongezewa thamani, zana za kilimo
-
7. Vituo Mahiri vya uhaulishaji Teknolojia
- TARI imeanzisha na kutumia Vituo Mahiri vya Uhaulishaji Teknolojia vinavyopatikana katika kanda zote nchini ili kuwezesha mkulima kujifunza kilimo bora kwa kuonea kwa vitendo, Vituo hivyo ni pamoja na Dkt. John Samwel Malecela (Dodoma), Mwalimu Julius Nyerere (Morogoro), Ngongo (Lindi), John Mwakangale (Mbeya), Themi (Arusha), Fatuma Mwasa (Tabora), Nyakabindi (Simiyu), Nyamhongolo (Mwanza) na Kyakailabwe (Kagera)
8. Ushirikiano na Huduma za Ugani
-
TARI inafanya kazi na Wizara, Taasisi, Idara, Tawala za Mikoa, Halmashauri, Mashirika Yasiyo ya kiserikali (NGOs), Makampuni na washirika wa maendeleo kufikia wakulima.
-
Pia inafikia wakulima kupitia mtandao wa ugani uliopo nchini.
9. Machapisho ya Utafiti
-
Matokeo ya utafiti huchapishwa katika majarida ya kitalaamu , vitabu, na ripoti za kitalaamu na za kisera ili kuwashauri watunga Sera na kubadilishana taarifa na marifa na watafiti, pamoja na washirika wa maendeleo.
10. Vikundi vya Kijamii
-
TARI inashirikiana na vikundi mbalimbali vya kijamii kama Vikundi vya Wakulima, na Vyama vya Ushirika kama njia za kujifunza miongoni mwa wakulima na kueneza matumizi ya teknolojia.
11. Teknolojia za Mawasiliano ya Simu na Mtandao
-
Matumizi ya huduma za ujumbe mfupi na simu za mkononi, programu za simu, na mifumo ya mawasiliano ya sauti kujibu maswali na kutoa ushauri wa kilimo kwa wakati halisi kwa wakulima na wadau.