Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

TARI ILONGA

Kituo cha Utafiti cha Ilonga ni miongoni mwa Vituo vya Utafiti wa Kilimo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kilichopo katika Wilaya ya Kilosa, mkoa wa Morogoro. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 1943, kikijulikana kama Kituo Kikuu cha Utafiti (CRC), kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa pamba katika Eneo la Ukulima wa Pamba Mashariki (ECGA). Mwaka 1989, kilibadilishwa kuwa Kituo cha Kanda kwa ajili ya Utafiti na Mafunzo katika Kanda ya Mashariki, hasa katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam.

Mnamo mwaka 2018, TARI ilizinduliwa rasmi kufuatia Sheria ya Bunge la Tanzania Na. 10 ya mwaka 2016, na Ilonga ikawa mojawapo ya vituo nane (8) vya TARI. Kituo hiki kina vituo vidogo viwili: Dakawa na Ifakara, vyote vikiwa katika mkoa wa Morogoro.


Muundo wa Kiutawala

Kituo kina idara kuu mbili:

  1. Utafiti na Ubunifu, inayoongozwa na Mratibu wa Kituo wa Utafiti na Ubunifu (CCRI)

  2. Uhamasishaji wa Teknolojia na Ushirikiano, inayoongozwa na Mratibu wa Kituo wa Uhamishaji Teknolojia na Ushirikiano (CCTTP)

Masuala ya rasilimali watu na utawala yanaratibiwa na Makao Makuu ya TARI kupitia kwa Mkurugenzi wa Kituo (CD).