Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

Research Labs

 TARI Referral Laboratory – Dodoma (Maabara Kuu ya Taifa)

Lengo kuu: Kutoa huduma za kitaalamu na sahihi kwa tafiti za kilimo, ufuatiliaji wa magonjwa, ubora wa mbegu, na uthibitishaji wa mazao.

 Sehemu Muhimu:

  1. Maabara ya Utambuzi wa Magonjwa:

    • Utambuzi wa magonjwa ya mimea kwa kutumia mbinu za kisasa (PCR, ELISA).

    • Kituo kikuu cha marejeo kwa afya ya mimea nchini.

  2. Chumba cha Uchimbaji wa Vina saba.

    • Uchimbaji wa DNA na RNA kutoka kwa mimea, mbegu, na vimelea.

  3. Chumba cha Utambuzi (Detection Room):

    • PCR na RT-PCR kwa ajili ya kugundua vimelea na upimaji wa vifaa vya kupandikiza.

  4. Maabara ya Upimaji Mbegu:

    • Viability, usafi, na uwezo wa kuota wa mbegu.

    • Upimaji wa magonjwa yanayobebwa na mbegu.

  5. Kitengo cha Usajili wa Mbegu:

    • Usajili, uchambuzi na ufuatiliaji wa sampuli za mbegu kwa mujibu wa viwango vya ISTA.

  6. Sehemu ya Usafi na Uotaji Mbegu:

    • Upimaji wa viwango vya usafi wa mbegu na uwezo wake wa kuota.

    • 8. Vyumba vya Uotaji Mbegu (Germination Chambers 1 & 2):

    • Mazingira yaliyoidhinishwa kwa ajili ya uotaji mbegu wa mazao mbalimbali.

TARI Mikocheni – Maabara ya Bioteknolojia

Kituo kikuu cha Taifa cha Utafiti wa Bioteknolojia ya Kilimo.

Maeneo Muhimu:

  • Utambuzi wa vimelea kwa njia za molekuli.

  • Usimamizi wa wadudu na vimelea kupitia vinasaba.

  • Characterization ya germplasm ya mazao: kahawa, muhogo, viazi vitamu, korosho n.k.

  • Tissue culture ya kupanda mimea safi na isiyo na magonjwa.

  • Uendelezaji wa bidhaa za kibayoteknolojia kama bio-pesticides na bio-fertilizers.

TARI Kibaha – Maabara ya Nematolojia na Molekuli

Kituo cha uchunguzi wa minyoo waharibifu na biocontrol.

Vitengo:

  1. Maabara ya Nematolojia:

    • Utambuzi wa minyoo kwa kutumia DNA.

    • Uchunguzi wa mwingiliano wa minyoo na mimea.

  2. Biocontrol kwa Wadudu (EPNs):

    • Uzalishaji wa EPNs kwa kudhibiti wadudu kama white grubs.

  3. Maabara ya Entomolojia:

    • Utafiti na utambuzi wa wadudu waharibifu na manufaa.

  4. Maabara ya Patholojia ya Mimea:

    • Utambuzi wa magonjwa ya miwa na mazao mengine kwa kutumia PCR.

  5. Tissue Culture ya Miwa na Muhogo:

    • Uzalishaji wa vipando visivyo na magonjwa.

 TARI Mlingano – Maabara ya Udongo na Tissue Culture ya Katani

Kituo kikuu cha Afrika Mashariki kwa sayansi ya udongo na katani.

1. Maabara ya Udongo:

  • Upimaji wa pH, EC, NPK, CEC, na micronutrients.

  • Uchoraji wa ramani za rutuba na matumizi ya ardhi kwa kutumia GIS.

  • Uchambuzi wa maji na mbolea.

2. Tissue Culture ya Katani:

  • Uzalishaji wa vipando safi vya katani.

  • Utafiti wa uhifadhi wa vinasaba na uboreshaji wa aina bora.

 TARI Uyole – Maabara ya Tissue Culture na Udongo

1. Tissue Culture Laboratory:

  • Uzalishaji wa viazi, ndizi, na pyrethrum kwa njia ya in vitro.

  • Uchunguzi wa magonjwa ya mimea kwa PCR/ELISA.

  • Uhifadhi wa germplasm.

2. Maabara ya Udongo:

  • Upimaji wa rutuba ya udongo (pH, NPK, micronutrients).

  • Uchoraji wa ramani za rutuba.

  • Mapendekezo ya matumizi ya mbolea.

  • Uchambuzi wa tishu za mimea na maji.

Faida kwa Taifa:

  • Kusaidia udhibiti wa magonjwa ya mimea.

  • Kuhakikisha ubora wa mbegu zinazozalishwa nchini.

  • Kuwezesha matumizi bora ya teknolojia ya kilimo (ICT, Bioteknolojia).

  • Kusaidia wakulima, watafiti, na taasisi katika kufanya maamuzi sahihi kulingana na data.