Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

TARI NA WADAU WAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA AFYA YA MIMEA.
13 May, 2026
TARI NA WADAU WAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA AFYA YA MIMEA.

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea katika viwanja vya John Samuel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, Mei 12, 2026.

Maadhimisho hayo yameratibiwa na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) chini ya kauli mbiu isemayo “Ulinzi wa Bayoanuai ya Mimea kwa Usalama wa Chakula na Lishe.” Siku hiyo huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Mei kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa afya ya mimea katika kuhakikisha usalama wa chakula na lishe, kukuza biashara na maendeleo endelevu duniani. Kwa mwaka huu, maadhimisho yalianza kwa maonesho tarehe 10 Mei na yamehitimishwa leo tarehe 12 Mei 2026, yakihusisha TARI na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo.

Akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) ambaye amemwakilishe Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo (Mb), amesema mimea ni msingi wa maisha duniani kwa kuwa ndiyo chanzo cha chakula, dawa pamoja na malighafi za viwandani.

Amesema Wizara ya Kilimo itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa TPHPA ili kuhakikisha huduma bora za usimamizi wa afya ya mimea zinaendelea kutolewa nchini kwa lengo la kukuza sekta ya kilimo na kufikia Agenda 10/30 pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha, Mhe. Silinde amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuimarisha huduma za kidijitali nchini, hatua ambayo imeendelea kuleta manufaa makubwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Silinde alisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi katika kulinda bayoanuai ya mimea kwa ajili ya kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Kwa upande wa TARI, iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu Dkt. Deusdedith Mbanzibwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, pamoja na Meneja wa Uhaulishaji Teknolojia, Biashara na Mahusiano, Dkt. Rajabu Joseph Kangile na watafiti mbalimbali kutoka TARI.

slot gacor