Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

TARI YASHIRIKI MAONYESHO YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU
18 Aug, 2026
TARI YASHIRIKI MAONYESHO YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imeshiriki katika Maonyesho ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa lengo la kuonesha teknolojia, tafiti na ubunifu mbalimbali zinazolenga kuboresha uzalishaji wa kilimo nchini.maonyesho yanayofanyika kuanzia tarehe 15 agosti,2026 hadi kilele tarehe 24 agosti,2026 katika viwanja vya shule ya sekondari Usagara,jijini Tanga yenye kauli mbiu “Elimu, Ujuzi na Ubunifu ,Njia ya kufikia Dira ya Taifa ya maendeleo 2050”

Katika maonyesho hayo, TARI imeshiriki kupitia vituo vyake vitatu ambavyo ni TARI Mlingano, TARI Naliendele,TARI Ukiliguru na TARI Tengeru. Vituo hivyo vimepata fursa ya kuonesha teknolojia na matokeo ya tafiti zinazoweza kuwasaidia wakulima Pamoja na wadau wengine wa sekta ya kilimo.

TARI  imewasilisha teknolojia na tafiti zinazohusiana na uzalishaji wa mazao, matumizi sahihi ya pembejeo na mbinu bora za kilimo zinazolenga kuongeza tija na kipato cha mkulima.

Kwa upande mwingine, TARI imeonesha teknolojia na ubunifu katika uzalishaji wa mazao yanayofanyiwa utafiti katika vituo hivyo ambazo ni Teknolojia za mbegu za mboga mboga mchicha akheri,poli na Nguruma,miche ya parachichi,stafeli na miche ya Vikolezo pamoja na mbegu za korosho,ufuta na karanga na bidhaa siagi,unga wa korosho na mvinyo unaotokana na mabibo,Teknolojia Unga wa muhogo,mihogo,Rafiki Planter  Pamoja na Teknolojia mpya ya Afya ya Kijani inayotumia Teknolojia ya akili unde (AI) kusaidia katika utambuzi wa magonjwa ya mazao itakayowawezesha wakulima kutambua magonjwa kwa haraka wakiwa shambani na kuchukua hatua stahiki kwa wakati kabla ya ugonjwa haujaenea na kusababisha Hasara kubwa kwa mkulima.

Maonyesho haya pia yametoa fursa kwa wananchi kupata elimu kuhusu teknolojia mpya za kilimo, kuuliza maswali kwa wataalamu na kujifunza namna ya kutumia teknolojia hizo katika kuongeza tija na kuboresha kipato cha mkulima.

TARI inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha utafiti, elimu, ujuzi na ubunifu vinatumika kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo na kuimarisha usalama wa chakula na kipato cha mkulima mmoja mmoja.