Karibu    
                                
                                
                                              
                            
   
                        Karibu katika tovuti ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kitovu cha Taifa cha ubunifu wa kilimo, ubora wa utafiti, na suluhisho endelevu kwa wakulima.
TARI tunaamini kuwa kilimo ndicho uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania na ufunguo wa kufikia usalama wa chakula, uhifadhi wa mazingira, na ukuaji jumuishi wa kiuchumi. Timu yetu yenye watafiti, wanasayansi, wahandisi na watumishi wenye kujituma inafanya kazi kwa bidii kote nchini ili kuendeleza na kusambaza teknolojia na mbinu bunifu zinazowawezesha wakulima na kubadilisha maisha ya vijijini.
Tukiwa na msingi imara wa kisayansi na dhamira thabiti ya kutoa huduma, tunajivunia kuongoza katika sekta ya utafiti na maendeleo ya kilimo. Iwe wewe ni mkulima, mtunga sera, mshirika wa maendeleo au mtafiti, tunakukaribisha kuchunguza kazi zetu, kuwasiliana na wataalamu wetu, na kuungana nasi katika kujenga sekta ya kilimo yenye tija na ustahimilivu zaidi kwa Tanzania na kwingineko.
Pamoja, tuikuze ubunifu kwa ajili ya kesho iliyo bora zaidi.
 
                        
