Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

Tari Yatoa Mbegu Bora za Miwa Kwa Wakulima Kilombero.
24 Nov, 2025
Tari Yatoa Mbegu Bora za Miwa Kwa Wakulima Kilombero.

TARI yatoa Mbegu bora za miwa kwa wakulima kilombero

 Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo chake cha TARI Kibaha imetoa zaidi ya tani 300 za mbegu bora za miwa aina ya R 570 kwa wakulima 60 wa Walaya ya kilombero mkoani Morogoro,ikiwa ni juhudi za kuongeza uzalishaji na kuinua kipato cha wakulima kupitia kilimo chenye tija.

Akizungumza wakati wa utoaji wa Mbegu hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Meneja wa Utafiti wa Rasilimali asili na Uhandisi Kilimo Dkt, Hildelitha Msita amesema  mbegu za R 570 zina ubora wa hali ya juu na zimekuwa zikionesha matokeo mazuri katika uzalishaji.

Dkt. Msita ameongeza kuwa kwa sasa wameanzisha shamba la uzalishaji wa mbegu za miwa Kijiji cha Ichonde kisawasawa,wilaya ya kilombero lenye ukubwa wa Ekari nne, ambalo linatarajiwa kuongeza upatikanaji endelevu wa mbegu bora kwa wakulima.

Aidha, Dkt. Msita, alitoa wito kwa wakulima kuhakikisha wanatumia mbegu za R 570 ili kuongeza tija,kuongeza mavuno na hatimaye kuboresha kipato cha mtu moja kwa moja.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe, Wakili, Dunstan Dominik Kyobya ameishukuru TARI kwa kugawa mbegu hizo huku akiwashauri Wananchi wa Kilombero kuchangamkia fursa ya kutumia mbegu bora zinazozalishwa na TARI kwa ajili ya kupata mavuno mengi na yenye tija.

Mmoja wa wanufaika wa mbegu hizo akiongea kwa niaba ya wakulima ndugu Yordan Nguruwe ameshukuru uongozi wa TARI Kwa kuwapatia mbegu bora na yenye tija kwani amesema itasaidia kuongeza kipato kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

 

 

HONGERA
Mh. Daniel Godfrey Chongolo

Kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo