Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara Ya Kilimo

TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA COP12 WA MKATABA WA NAIROBI
12 Oct, 2026
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA COP12 WA MKATABA WA NAIROBI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, Oktoba 8, 2026, jijini Dar es Salaam, amefungua Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika uhifadhi wa mazingira ya bahari na pwani, pamoja na kuendeleza uchumi endelevu wa buluu. Unawakutanisha wajumbe zaidi ya 500 kutoka nchi 10 wanachama wa Mkataba wa Nairobi pamoja na washirika mbalimbali wa maendeleo na taasisi za kimataifa.

Katika mkutano huo, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inaendelea kutoa elimu kwa wadau kuhusu matumizi ya teknolojia za kilimo zinazozingatia uhifadhi wa mazingira. Elimu hiyo inajikita katika matumizi sahihi na endelevu ya rasilimali za maji, pamoja na matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira katika shughuli za uzalishaji wa kilimo.

Kupitia ushiriki huo, TARI inalenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu namna teknolojia za kilimo zinavyoweza kutumika kuongeza tija na uzalishaji wa mazao huku zikizingatia matumizi endelevu ya rasilimali za maji na kulinda mazingira.

Ushiriki wa TARI katika COP12 ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha matumizi ya teknolojia bunifu za kilimo, usimamizi endelevu wa rasilimali za asili na uhifadhi wa mazingira, kwa lengo la kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo na Taifa kwa ujumla.

slot gacor